Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi Winnie

Sikukujua Winnie zaidi ya chat za facebook Bongo real mamaz, ila kifo chako kimenisikitisha sana sana sana. inakuwaje mpaka leo wanawake wa AFRIKA bado wanafariki wakati wa kujifungua? jamani serikali yetu tafadhali agalizo katika eneo hili la uzazi wa kina mama?? ? je madaktari wazembe wanaosababisha vifo hivi kwanini hawawajibishwi? uchungu wangu ni mkubwa sana, nalia na familia zote zilizokwisha poteza mama au mtoto kipindi cha uzazi. Mungu awatie nguvu na amani tele. tuko pamoja kwa maombi.

No comments: